Get Adobe Flash player

NAFASI ZA MASOMO KWA 2014 - 2015

Taarifa kwa Umma:Muda wa kutuma maombi umeongezwa hadi kufikia Tarehe 18 July 2014 saa 11 Jioni siku ya Ijumaa

Chuo cha madini Shinyanga kinatangaza nafasi za masomo kwa muhula wa 2014/2015 utakaoanza Agosti 2014 katika ngazi ya cheti na diploma katika fani za:

 1. Utafutaji na Jiolojia ya Uchimbaji wa Madini (CERTIFICATE AND DIPLOMA IN EXPLORATION AND MINING GEOLOGY)
 2. Utafutaji na Jiolojia ya Uchimbaji wa Mafuta na Gesi (CERTIFICATE AND DIPLOMA IN PETROLEUM GEOLOGY)
 • Chuo kipo ndani ya MGODI WA MWADUI na kimesajiliwa na NACTE kwa namba REG/EOS/041P.
 • Ada pamoja na malazi kwa mwaka ni Shs. 1,783,000
 • Fomu za maombi zinapatikana katika ofisi za chuo zilizopo Ndala block HH No.91 Shinyanga  mjini.
 • Pia fomu zinapatikana katika tovuti yetu ya www.esis.ac.tz
 • Maombi yanapokelewa kuanzia 1 April 2014 hadi 30 Juni 2014

Kwa maelezo na taratibu fuata kiunganishi hiki: http://esis.ac.tz/application-admission/application-process/

Karibuni nyote

Kuna njia mbili za kuomba

 1. Online application
 2. Offline application

Kwa wale wanaotaka kujaza hapa hapa bofya hapa chini:

Online Application Form No. 1

Online Application Form No. 2

Kwa wale wanaotaka kutuma kwa posta pakua hapa downloadable form

Masharti ya kutuma maombi

Cheti ya mwaka mmoja

 • Mwombaji awe angalau na D nne katika matokeo yake ya kidato cha nne AU
 • Awe amefaulu NVTA 3 (Certificate of Competence – Level III) kutoka VETA kwa masomo ay uhandisi

Diploma ya miaka miwili

 • Awe amesoma na kufaulu NTAL4 (cheti kutoka chuo kilichosajiliwa na  NACTE )

Ada ya maombi ni Shs.  25,000/ (Ada hii hairudishwi)

Soma zaidi – Taratibu za kuomba

Mwisho wa kutuma Maombi yameongezwa hadi Tarehe 18 Julai 2014 11 Jiioni

Maombi yako tuma kwa

Mkuu wa Chuo,

Chuo cha Madini Shinyanga

SLP 1016,

Shinyanga, Tanzania